Romans 9

1Nasema ukweli katika Kristo. Sisemi uongo, na dhamira yangu hushuhudia pamoja nami katika Roho Mtakatifu, 2kwamba kuna huzuni kubwa na maumivu yasiyo koma ndani ya moyo wangu.

3Kwamba ningetamani mimi mwenyewe kulaaniwa na kutengwa mbali na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu, wale wa jamii yangu katika mwili. 4Wao ni Waisraeli. Walio na hali ya kufanyika watoto, wa utukufu, wa maagano, na zawadi ya sheria, kumwabudu Mungu, na ahadi. 5Wao ni watangulizi ambako Kristo amekuja kwa heshima kuvaa mwili huu - ambaye yeye ni Mungu wa vyote. Naye asifiwe milele. Amina.

6Lakini si kwamba ahadi za Mungu zimeshindwa kutimia. Maana si kila mtu aliye Israeli ni Mwiisraeli halisi. 7Sivyo hata kwa uzao wa Abrahamu kuwa ni watoto wake halisi. Lakini, “ni kupitia Isaka uzao wako utaitwa.”

8Hii ni kwamba, watoto wa mwili si watoto wa Mungu. Lakini watoto wa ahadi wanatazamwa kuwa kama uzao. 9Maana hili ndilo neno la ahadi: “Katika majira haya nitakuja, na Sara atapewa mtoto.”

10Si hili tu, lakini baada ya Rebeka kupata mimba kwa mtu mmoja, Isaka baba yetu- 11kwamba watoto walikuwa bado hawajazaliwa na alikuwa hajafanya jambo lolote zuri au baya, ili kwamba kusudi la Mungu kulingana na uchaguzi lisimame, wala si kwa matendo, lakini ni kwa sababu ya yule aitae. 12Ilinenwa kwake, “Mkubwa atamtumikia mdogo.” 13Kama ilivyo kwisha andikwa: “Yakobo nilimpenda, lakini Esau nilimchukia.”

14Basi tena tutasema nini? Je kuna udhalimu kwa Mungu? La hasha. 15Kwa kuwa anasema kwa Musa, “nitakuwa na rehema kwa yule nitakayemrehemu, na nitakuwa na huruma kwa yule nitakayemhurumia.” 16Kwa hiyo basi, si kwa sababu ya yeye atakaye, wala si kwa sababu ya yeye ambaye hukimbia, lakini kwa sababu ya Mungu, ambaye huonesha rehema.

17Kwa kuwa maandiko husema kwa Farao, “Kwa kusudi hili maalumu nilikuinua, ili kwamba nioneshe nguvu zangu katika wewe, na ili kwamba jina langu litangazwe katika nchi yote.” 18Hivyo basi, Mungu huwa na rehema kwa yeyote ampendaye, na kwa ambaye humpenda, humfanya kuwa mkaidi.

19Kisha utasema kwangu, “Kwa nini bado anaona kosa? Ni yupi ambaye alikwisha kustahimili matakwa yake?” 20Kinyume chake, mwanadamu, wewe ni nani ujibue kinyume na Mungu? Kuna uwezekano wowote wa kilichofinyangwa kusema kwa mfinyanzi, “Kwanini ulinifanya hivi mimi?” 21Je mfinyazi huwa hana haki juu ya udongo kutengeneza chombo kwa matumizi maalumu kutokana na bonge lile lile, na chombo kingine kwa matumizi ya kila siku?

22Vipi kama Mungu, ambaye ana utayari wa kuonesha gadhabu yake na kufanya nguvu yake kujulikana, alistahimili kwa uvumilivu wa kutosha vyombo vya gadhabu vilivyoandaliwa kwa kuangamiza? 23Vipi kama alifanya hivi ili kwamba aoneshe wingi wa utukufu wake juu ya vyombo vya rehema, ambavyo alikwisha kuviandaa kwa ajili ya utukufu? 24Vipi kama alifanya hii pia kwetu, ambaye pia alituita, si tu kutoka kwa Wayahudi, lakini pia kutoka kwa watu wa Mataifa?

25Kama asemavyo pia katika Hosea: “Nitawaita watu wangu ambao hawakuwa watu wangu, na mpendwa wake ambaye hakupendwa. 26Na itakuwa kwamba pale iliposemwa kwao, ‘Ninyi si watu wangu,’ pale wataitwa ‘wana wa Mungu aliye hai.”’

27Isaya analia kuhusiana na Israeli, “Kama hesabu ya wana wa Israeli ingekuwa kama mchanga wa bahari, itakuwa ni masalia ambao wataokolewa. 28Kwa kuwa Bwana atalichukua neno lake juu ya nchi, mapema na kwa utimilifu. 29Na kama jinsi Isaya alivyosema awali, “Kama Bwana wa majeshi hakutuachia nyuma uzao kwa ajili yetu, tungekuwa kama Sodoma, na tungefanywa kama Gomora.

30Tutasema nini basi? kwamba watu wa Mataifa ambao walikuwa hawatafuti haki, walipata haki, haki kwa imani. 31Lakini Israeli, ambaye alitafuta sheria ya haki, hakuifikia.

32Kwanini si hivyo? Kwa sababu hawakuitafuta kwa imani, bali kwa matendo. Walijikwaa juu ya jiwe la kujikwaa, kama ilivyo kwisha andikwa, “Tazama, nimelaza jiwe la kujikwaa katika Sayuni na mwamba wa kukosa. Yeye ambaye huamini katika hili hataaibika.”

33

Copyright information for SwaULB